Zidane amegombana na Rais wa Real Madrid, kisa ?


Julya 19 2016 headlines za kocha na staa wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidanezimekuwa stori kubwa mitandaoni, Zidane anaripotiwa na mtandao wa dailyamail.co.ukkuwa ametofautiana na Rais wa klabu ya Real Madrid Fiorentino Perez.
Perez na Zidane wanatajwa kupishana kutokana na Zidane kutokuwa tayari kumjumuisha kinda Martin Odegaard katika kikosi chake kinachoanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu, Zidane ametaja kutaka kumuacha Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 17 kutokana na maendeleo yake kikosini kuwa tofauti na matarajio.
Zidane-and-Perez
Kutoka kushoto ni Zidane na Perez
Sababu nyingine inayomfanya Zidane amuache mchezaji huyo katika kikosi chake ni kutokana kutokuwa na mipango nae katika msimu huu, hivyo alikuwa anataka arudi katika kikosi cha wachezaji wa akiba Castilla.

No comments

Powered by Blogger.